OMAR ZONGO

Naitwa Omar Zongo ni Mtangazaji na unaweza kunisikia Jumatatu mpaka
Ijumaa saa 11 asubuhi mpaka saa 12 asubuhi katika kipindi cha Eastafrica
Breakfast.
Nipo kwenye tasnia ya habari kwa miaka kadhaa nikiwa nimebobea kwenye
Habari na Matukio.

Kinachonivutia kwenye fani ya Habari na Utangazaji ni kuwa karibu na
watu nakujifunza vitu vipya kila wakati.

Nje ya taaluma yangu ya habari na mawasiliano pia ni mtunzi wa Riwaya,
Tamthilia na maigizo ya jukwaani.
Napenda kutazama movies lakini zaidi napenda kusoma vitabu vya hamasa na
Historia.