SCOLAR KISANGA

Naitwa Scolar Kisanga na ni mtangazaji wa kipindi cha East Africa Breakfast pia na Weekend Breakfast (kila Jumamosi). Nilimaliza shahada ya kwanza ya mawasiliano ya Umma katika chuo kikuu cha Mt.Agustion SAUT( B.A in mass Comunication)
Nikaanza kazi za utangazaji rasmi tangu mwaka 2011 wakati alipojiunga mwaka wa kwanza kwatika chuo cha Mt.Agustino Mwanza nikifanya kazi na redio Saut Fm kwa miaka mitatu mfululizo na baadae kuajiriwa rasmi na Media house nyingine.
Nilipenda Fani ya utangazaji tangu nikiwa mtoto ambapo nilikuwa nikivutiwa na watangazaji wakongwe katika miaka ya 90 mpaka 2000 na nilikuwa mpenzi mkubwa sana na msikilizaji mzuri wa radio.
Nilivyokuwa shuleni katika kidato cha tano na cha sita nilikuwa mshereheshaji wa shule (MC) katika shule ya sekondari Mawenzi (Moshi) wakati nikiendelea kukuza kipaji changu cha utangazaji.
Lakini pia ni muigizaji, mcheshi na hupenda kuzungumza na kila mmoja na ni rafiki wa wengi.
Najuvunia sana sana kuwa na KIPAJI cha utangazaji na sikuwahi kujuta hata mara moja kuichagua fani hii.... Binafsi nina usemo niliojipa unaosema My Career To Death, Baada ya mapenzi yangu kwa Mungu Muumba, Baba yangu mzazi basi kinachofuata ni Kipaji (KAZI) yangu binafsi ya UTANGAZAJI