ZEMBWELA

Zembwela (Hillary Daudi) ni mwandaaji na mtangazaji wa East Africa Radio mwenye sifa ya ucheshi, ukarimu na mwenye kupenda urafiki na watu wa kada mbali mbali.Pia ni mchekeshaji ambapo kabla ya kujiunga na East Africa Radio alijulikana na wengi kwa mchango wake wa kuelimisha jamii kupitia michezo ya kuigiza na ucheshi.Mbali ya kipindi cha Supa Mix, Zambwela pia ni mtangazaji wa kipindi maarufu cha televisheni Cha Uswazi na pia amekuwa akionyesha vipaji vyake kupitia kazi za uandaaji na ushehereshaji (MC) wa matamasha na sherehe mbali mbali.